Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ashtakiwa kwa Kumuibia Mpenziwe Simu ya KSh 140k, Pasipoti

  • Msichana huyo alikutana na mpenzi wake mpya siku mbili tu kabla ya wizi huo
  • Kulingana na mwathiriwa, mwanamke aliyekuwa na msichana huyo wa chuo kikuu alitoweka na simu, pasipoti na pesa zake zote za thamani ya KSh 262,440
  • Mshukiwa, Veronica Njeri alikanusha mashtaka mbele ya hakimu Esther Boke katika mahakama ya Kibera

Mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja nchini Kenya kwa sasa anajuta baada ya kujipata gerezani aliponaswa kwa kumuibia mwanadiplomasia wa Sierra Leone.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ashtakiwa kwa Kumuibia Mpenziwe
Mwanamke huyo alikuwa amemjua mwanamume aliyemwibia pesa kwa siku mbili tu. Picha: UGC.
Source: UGC

Veronica Njeri, mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja humu nchini, alishtakiwa kwa kumuibia mwanamume huyo mpenziwe aliyetambulika kama Kabba Ibrahim simu ya KSh 140,000.

Kulingana na Nairobi News, Veronica pia aliiba pasipoti ya Kabba na pesa taslimu zote za thamani ya KSh 262,440.

Veronica, 23, aliripotiwa kuwa pamoja na msichana mwingine ambaye bado hajatambulika walipodaiwa kutekeleza uhalifu huo Jumatatu, Novemba 8, katika nyumba ya Black Rose.

Polisi waliarifiwa kuwa Veronica, mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Nairobi alimpigia simu Kabba na kumuarifu kwamba alikuwa amelewa sana na alihitaji usaidizi wake.

Read also

Embu: Babu Amuua Mkewe Aliyetoweka na KSh 6000, Kurejea Akiwa Mlevi

Kabba ambaye alimfahamu Veronica kwa siku mbili tu alikimbia eneo alilokuwemo na kumkuta akiwa na mwenzake wake ambaye alimwarifu kwamba alikuwa rafiki yake.

Akitumia teksi, Kabba aliwachukua wote wawili Veronica na rafiki yake hadi nyumbani kwake, ambapo uhalifu ulitokea.

Baada ya kufika nyumbani kwake, alimuacha mgeni huyo sebuleni kwake na kumpeleka Veronica kwenye choo ambapo walitumia takribani dakika 10 mshukiwa akitapika.

Dada ambaye aliachwa ndani ya nyumba hata hivyo alitoweka kabla ya wawili hao kurejea.

Hata hivyo, aliiacha nyuma simu yake ambayo alikuwa ameondoa kadi.

Veronica akiwa amelala Kabba alielekea kituo cha polisi ambako aliandikisha taarifa.

Siku moja baadaye, Veronica aliwaambia polisi kuwa hamfahamu mwanamke aliyekuwa naye alipompigia simu Kabba kumchukua katika kilabu kilichoko mtaani Kilimani, Nairobi.

Polisi walimkamata na kumfungulia mashtaka ya wizi.

Msichana huyo wa chuo kikuu alikanusha mashtaka mbele ya hakimu mkuu mkuu Esther Boke katika mahakama ya Kibera.

Aliachiliwa kwa bondi ya KSh 300,000 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho na dhamana mbadala ya pesa taslimu KSh 100,000.

Read also

Mlaghai wa Mapenzi Akamatwa Baada ya Kuwadanganya Wanawake Atawaoa

Kesi hiyo itatajwa Jumatano, Novemba 24.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Source: Tuko

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here