Mpango wa Miguna wa Kurejea Nchini Wapata Pigo Baada ya Mahakama Kudinda Kuondoa Agizo Linalomzuia Kurudi

  • Miguna Miguna aliitaka tahadhari iliyotolewa na serikali ya Kenya kwa shirika la ndege la Ujerumani la Lufthansa na shirika la ndege la Ufaransa, kuondolewa na jaji wa mahakama kuu
  • Hedwig Ongudi alidinda kutoa agizo hilo baada ya wakili Miguna kutaka vikwazo vya kurejea kwake wiki ijayo humu nchini, viondolewe na mahakama
  • Ndege iliyopangwa kumbeba Miguna ilitarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) asubuhi ya mwezi Novemba 16

Safari iliyosubiriwa kwa hamu na gamu ya kurejea kwa wakili Mkenya anayeishi Canada, Miguna Miguna inaonekana imetibuka baada ya mahakama kuu kudinda kutoa agizo linalomzuia kurudi humu nchini.

Mpango wa Miguna wa Kurejea Nchini Wapata Pigo Baada ya Mahakama Kudinda Kuondoa Agizo Linalomzuia Kurudi
Wakili Mkenya anayeishi Canada Miguna Miguna huenda akakosa kurejea nchini baada ya mahakama kuu kukosa kuondoa agizo linalomzuia kuingia nchini. Picha: Miguna Miguna.
Source: Twitter

Runinga ya Citizen TV iliripoti kwamba jaji wa mahakama kuu Hedwig Ongudi alidinda kuondoa agizo hilo baada ya wakili kutaka vikwazo vilivyotolewa dhidi yake kutupiliwa mbali ili aweze kurejea Kenya wiki ijayo.

Ndege iliyopaswa kumbeba Miguna ilitarajiwa kutua uwanjwa wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) ausbuhi ya Novemba 16.

Read also

Kisanga Kaburi Likifunikwa Usiku Mama Akikataa Kumzika Mwanawe wa Kambo Aliyeangamia Limuru

Miguna aliitaka tahadhari iliyotolewa na serikali ya Kenya kwa mashirika mawili ya ndege ya Lufthansa na Ufaransa, kuondolewa ili aweze kusafiri hadi Kenya.

Ongudi alisema Miguna alipaswa kuwasilisha ushahidi ambao ungethibitisha kuwa serikali ilikuwa imetoa tahadhari hiyo na iwapo kweli tahadhari hizo zingalipo.

Wakili John Khaminwa kwa niaba ya Miguna, alikuwa amewasilisha ombi kwa mahakama kuu akidai kwamba tahadhari hiyo ilisababisha iwe vigumu kwa mteja wake kuingia humu nchini.

Miguna alishikilia kwamba tahadhari hiyo sio halali na kwamba inapaswa kutupiliwa mbali ili aruhusiwe kuendelea na safari yake. Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali ombi hilo, ikisema kwamba haiwezi kutegemea madai ya uvumi.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Source: Tuko Breaking News Latest

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here